Swahili

USHINDI WA BARACK OBAMA CHANGA MOTO KWA VIONGOZI WA AFRICA

Ushindi wa Barack Obama ulipokelewa kwa vishindo na mataifa ya Afrika na ulimwengu mzima. Ushindi wa Barrack Obama ni changamoto kubwa kwa viongozi wa Afrika ambao uongozi wao umekumbwa na kasumba kali za ufisadi na matumizi mabaya ya mali ya uma. Ushindi wa Barack Obama kama rais wa 44 wa Amerika ni ishara kwamba yote ya wezekana mradi tu uwe na bidii na motisha maishani.

Kutokana na ushindi huo, viongozi wa Afrika wana matarajio chungu mzima kutoka kwa rais mteule Barack Obama. Kile ambacho viongozi wa Afrika wana stahili kujuwa nikwamba kuwa rais wa kwanza wa asili ya kiafrika wa merekani si suluhu kwa shida zinazokumba bara la Afrika. Matatizo ya mataifa ya Afrika yanatokana na sera mbaya za uongozi na viogozi wasio kuwa na maono, ufisadi serikalini, unyanyasaji wa wananchi, na demokrasia isiyo na maadili mema.

Hali hiyo imechangia uharibifu wa miundo msingi ya mataiifa ya kiafrika na kuleta umasikini katika Jamii. Umasikini umekithiri na kukolea katika bara la Afrika kwa kiwango kikubwa sana, baa la njaa, ukosefu wa chakula, elimu duni, na ukosefu wa miundo mbiu (msingi)ni ishara kwamba viongozi wa Afrika wamelegea kimaendeleo na kustawi katika sanaa ya kubugia mali ya uma.

Shida zinazo kumba baadhi ya inchi za Afrika sio tatizo la Barack Obama kama vile tunavyo tarajia kutokana na ushindi wake tutataua shida izo, ni jambo la msingi viongozi wa mataifa ya Afrika kutilia mkazo maadili mema serikalini kwa kutumia vyema raslimali na kuboresha uchumi wa mataifa maskini. Afrika tuna rasli mali za kuboresha nguvu za dola na ili kuwezesha nguvu za dola kutoa uduma bora kwa mwananchi kwa kuzingatia sekta muhimu za ujenzi wa taifa kama vile elimu, uboreshaji wa miundo mbiu(msingi), ukulima, and soko huru. Kwa hivyo ushindi wa Obama usiwe tarajio kubwa kwa Afrika kwa sababu yeye ni rais wa Amereka na sio Afrika bali tu mjukuu wa Afrika na kiongozi wa taifa lenye uwezo mkubwa duniani.

Leave a comment